>

BETPAWA YATUMIA 69.3 MILIONI KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI NANGOMA, MTWARA

KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya betPawa imetumia jumla ya Sh 69.3 millioni kukamilisha ujenzi na uboreshwaji wa zahanati ya kijiji cha Nangomba ya mkoani Mtwara.

Fedha hizo zimetimika katika ujenzi, uboreshaji na upanuzi wa zahanati hiyo kupitia programu ya Dream Maker yenye lengo la kusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii nchini.

Meneja Masoko kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya betPawa, Borah Ndanyungu amesema kuwa wanajisikia fahari kushiriki katika jamii hasa sekta ya afya na kutatua tatizo hilo kwa kijiji cha Nangomba.

Ndanyungu alisema kuwa hatua ya kuboresha zahanati imetokana na maombi yaliyowasilishwa na Ofisa Tabibu,  Anania Muba kupitia program ya Dream Maker ambayo mpaka sasa imetatua  changamoto mbalimbali 20  katika jamii,

 “Uboreshwaji huo ni pamoja na kukarabati kuta zilizoharibika, kuinua urefu wa jengo, kuongeza mihimili na kumalizia kupiga  plasta, kuweka milango, tiles, kupaka rangi kuta na kufunga madirisha ya kisasa ya Aluminum,” amesema  Borah..

Alisema kuwa Muba  aliwasiliana na betPawa kupitia mradi wa Dream Maker, akitafuta usaidizi katika kukamilisha ukarabati wa kituo cha umma baada ya maendeleo yake kukwama.

“Mpaka zaidi ya Sh 500 milini zimetumika kusaidia jamii kupitia program ya Dream Maker na fedha hizo zimetumika kwa miezi 10. Programu ya Dream Maker ni mkakati wa kampuni yetu katika kusaidia jamii.

“Ni ndoto za upendo kama hizi zinazotuhamasisha na kuendesha mradi wa Dream Maker kwa sababu tunajua kwamba pamoja tunaweza kuleta mabadiliko ya kudumu na chanya kwa kila jamii kwa wakati mmoja,” amesema.

Kwa upande wake, Muba amesema kuwa ndoto yake kubwa ilikuwa kukamilisha ukarabati na upanuzi wa kliniki  yao ambayo inatoa huduma kwa wakazi zaidi ya 9,785.

“Jengo tulilokuwa tukilitumia hapo awali lilikuwa katika hali mbaya na halikuwa salama kutumika kama kituo cha afya. Nashukuru betPawa kwa kufanya ndoto yangu kuwa kweli kwa kukubali ombi langu ndani ya muda mfupi. Wakazi wa Ndangoma na maeneo jirani kwa sasa wanaweza kufurahia huduma katika mazingira ya kisasa, salama na ya usafi,” amesema Muba.

Kwa upande wake, Diwani wa Nangomba, Bw Sijaona Athumani aliipomgeza kampuni ya betPawa kwa kufanikisha mradi huo kutoa wito kwa  kampuni mbalimbali kuiga mfano wa kamupuni hiyo kwa changamoto katika jamii bado ni nyingi.

 “Nifuraha kuweza kuona zahanati hii itahudumia idadi ya wananchi wasiopungua 9,785 wakitokea sehemu mbalimbali hapa kijijini. Naishukuru betPawa kwa kutufanikishia ujenzi na uboreshwaji wa kituo hiki. Bw Muba ameonyesha uzalendo wake kwa wakazi wa Ndangoma, naomba kila mmoja aige mfano wake,” amesema Athumani.