>

NGAO YA JAMII LIGI YA WANAWAKE KINAWAKA KMC MWENGE

KARIAKOO Dabi ya Wanawake inatarajiwa kupigwa leo Uwanja wa KMC, Mwenge huku timu zote zikitamba kufanya vizuri kwenye msako wa ushindi wa Ngao ya Jamii 2024.

Ikumbukwe kwamba ni Simba Queens hawa ni mabingwa watetezi wa taji hilo ambalo walitwaa 2023 hivyo watakuwa kazini kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Yanga Princess.

Mussa Mgosi, kocha msaidizi wa Simba Queens amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na malengo yao ni kuvunja rekodi yao wenyewe ndani ya uwanja.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Yanga Princess na malengo yetu ni kuvunja rekodi yetu wenyewe hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu muhimu.”

    Kocha wa Yanga Princess Edna Lema kuhusu mchezo wao dhidi ya Simba Queens utakaochezwa saa 10 jioni Uwanja wa KMC, Mwenge amesema kuwa wapo tayari kupambana kwenye mchezo huo mgumu.

“Ni mchezo mgumu ambao upo mbele yetu hasa ukizingatia ni Kariakoo Dabi hivyo tunakwenda kufanya kazi kubwa kutafuta ushindi inawezekana, tupo tayari kwa mchezo huo.”

Mbali na Kariakoo Dabi kwa Wanawake kuna mchezo wa Ngao ya Jamii nusu fainali ya kwanza ambayo nayo itachezwa kesho Uwanja wa KMC mapema kati ya Ceasiaaa Queens dhidi ya JKT Tanzania.

Kocha wa Ceasiaa Queens Shabani Said amesema kuwa wamefanya maandalizi mazuri kuwakabili wapinzani wao JKT Queens kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa leo saa 7 mchana uwanja wa KMC, Mwenge.

Mchezaji wa Ceasiaa Queens Tausi Abdallah amesema kuwa watawapa furaha mashabiki wa Iringa kwenye mchezo huo kutokana na kufanya maandalizi mazuri.

Kocha wa JKT Queens Ester Chabruma amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo wao wataingia kwa tahadhari kuwakabili wapinzani wao.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kuipata 0756 028 371.