WAKIWA Uwanja wa Jamhuri, Dodoma wachezaji wa Simba na benchi la ufundi limeshuhudia ubao ukisoma Dodoma Jiji 0-1 Simba baada ya dakika 90 kugota mwisho.
Huu ni mchezo wa kwanza Simba kukamilisha dakika 45 bila kupata bao la kuongoza na wapinzani wao pia kutopata bao ndani ya dakika 45 za mwanzo. Beki wa kati wa Dodoma Jiji ambaye aliwahi kucheza Simba alipiga kazi kwa kushirikiana na wachezaji wengine wa Dodoma Jiji kuizuia safu ya ushambuliaji ya Simba iliyokuwa inaongozwa na Leonel Ateba.
Bao pekee la ushindi limefungwa na Jean Ahoa dakika ya 63 kwa pigo la penalti baada ya mwamuzi kuamuru ipigwe penalti baada ya kutafsri kuwa nahodha Mohamed Hussen Zimbwe Jr alikuwa amechezewa faulo ndani ya 18 na nyota wa Dodoma Jiji.
Ni bao la pili Ahoa anafunga ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25 huku Simba ikifikisha pointi 12 baada ya kucheza mechi nne za ligi ikishinda zote.
Ikumbukwe kwamba Ahoua ambaye ni ingizo jipya ndani ya Simba anakuwa mchezaji wa pili kuifunga Dodoma Jiji kwa hivi karibuni kwenye mchezo wa kwanza kukutana nao uwanjani kama ilivyokuwa kwa Jean Baleke ambaye msimu wa 2022/23 mchezo wake wa kwanza kucheza dhidi ya Dodoma Jiji alifunga bao dakika ya 45 kwa pasi ya Kibu Dennis.
Nyota wa mchezo amechaguliwa Deborah Mavambo ambaye alianza kikosi cha kwanza na kukomba dakika 90 kwenye mchezo uliochezwa Septemba 29 2024.
Ni nafasi ya tatu kwenye msimamo Simba ipo baada ya kufikisha pointi 12 vinara ni Singida Black Stars wenye pointi 13 kwenye msimamo wa ligi.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kuipata 0756 028 371.