>

GANZI YA MAUMIVU KWENYE UPENDO YAPIGA HODI KIGAMBONI

RASMI ile simulizi ya Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo iliyopata nafasi ya kutoka kwenye gazeti la Championi Jumatano na kusomwa na zaidi ya Watanzania milioni sasa inapiga hodi Kigamboni mji ulitulia huku amani ikizidi kutawala kila kona.

Ikumbukwe kwamba hii ni simulizi ya kwanza kuwa kwenye mfumo wa kitabu imeandikwa na Mtunzi Lunyamadzo Myuka, A Boy From Njombe Place To Be  ipo tayari mtaanirasmi ilitambulishwa Septemba 24 2024 na mapokezi yake yamekuwa mazuri ikianza kupatikana kwa wakazi wa Dar na vitongoji vyake.

Wakazi wa Sinza Mori, Mbagala, Kigamboni, Goba, Sinza Kumekucha, Bamaga tayari wameanza kupata nakala zao ambapo namba ya oda ni 0756 028 371 hapo ulipo inakufikia na unaweza kufika pia makao makuu ya Global Group, Sinza Mori Dar kupata kitabu cha Ganzi ya Maumivu pamoja na vitabu vya Legendi kwenye utunzi wa hadithi Eric Shigongo.

Ni zamu ya Kigamboni, Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo inapiga hodi kuwafikiwa wasomaji wake ambao waliisoma pia ilipokuwa kwenye nakala ya Championi muda ni sasa ambapo wakazi wa Kigamboni waliisubiri kwa shauku kubwa na muda wa kuipata simulizi hiyo umefika.

Simulizi hiyo inazungumzia maisha halisi ya Kiafrika huku ikitoa somo kuhusu atahari za madawa ya kulevya, athari za makundi bila kusahau visasi na upendo.

Hii ni kwa ajili yako hakika ukiipata nakala hii hautajuta utarudi kunishukuru baadaye. Imehaririwa na Omary Mdose, Minaj, Mhakiki wa Simulizi hiyo ni Mwandishi Bora mwenye tuzo ya uandishi Bongo Joseph Shaluwa ambaye pia kasimamia kwenye masuala ya chapa ya kwanza ya kitabu hicho na msanifu kurasa ni Bahati Haule.