>

AZAM FC YAPOTEZA MCHEZO WAKE WA KWANZA BONGO

MATAJIRI wa Dar Azam FC msimu wa 2024/25 wamepoteza mchezo wa kwanza wakiwa ndani ya Uwanja wa New Amaan Complex mbele ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Azam FC ilikuwa imecheza jumla ya mechi nne ambazo ni dakika 360 bila kuambulia kichapo kwenye mechi hizo ambapo ilipata ushindi kwenye mechi mbili na kuambulia sare kwenye mchezo mmoja.

Ilikuwa JKT Tanzania 0-0 Azam FC, Azam FC 0-0 Pamba Jiji kwenye mechi hizi ilitoshana nguvu na mpinzani wake na mchezo dhidi ya KMC 0-4 Azam FC, Azam FC 1-0 Coastal Union ilikomba pointi tatu hivyo kwenye mechi nne ni mabao matano ilifunga na kinara wa kutengeneza pasi za mwisho ni Feisal Salum mwenye pasi tatu  ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora dhidi ya KMC.

Mchezo wa kwanza kupoteza ilikuwa Septemba 26 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 0-2 Simba mabao yakifungwa na Leonel Ateba dakika ya 14 na Fabrince Ngoma dakika ya 47 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.

Simba imecheza jumla ya mechi tatu msimu wa 2024/25 ikikomba pointi tisa na safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 9 ambapo mchezo walioshinda mabao mengi ilikuwa dhidi ya Fountain Gate, Uwanja wa KMC, Complex walishinda mabao 4-0.

Na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, 0756 028 371 kukipata