WAKATI ikiwa ni saa chache zimesalia kabla ya ulimwengu wa mpira kushuhudia Mzizima Dabi Uwanja wa New Amaan Complex, pilato wa mchezo huo weka mbali na watoto kutokana na misimamo yake akiwa kwenye majukumu yake.
Azam FC itawakaribisha Simba kwenye mchezo wa kwanza msimu wa 2024/25 ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Herry Sasy ni moja ya waamuzi ambao wamekuwa makini kwenye kutimiza majukumu yao licha ya makosa ya kibinadamu hivyo hayo yote ni lazima washirikiane kwa pamoja na timu nzima ya waamuzi kutimiza majukumu kwa umakini kwa kuwa huu mchezo unaushindani mkubwa na unafuatiliwa na wengi duniani.
Ipo wazi kwamba utakuwa mubashara Azam TV ikiwa inamaanisha kwamba dunia inashuhudia burudani na maamuzi ya Sasii yatakuwa yakitazamwa pia akitimiza sheria 17 za mpira.
Sasii atasaidiwa na Mohamed Mkono na Zawadi Yusuf wote wakitokea Dar na Kamishna wa mchezo huo ni Cyprian Kuyava kutoka Iringa huku mwamuzi wa akiba ni Amina Kyando kutoka Dar.
Imeandikwa na Lunyamadzo Myuka, Mtunzi Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kuipata 0756 028 371.