NADO MZEE WA REKODI NDANI YA AZAM FC

MWAMBA Idd Suleiman Nado ni mzee wa rekodi ndani ya Azam FC kwenye msimu mpya wa 2024/25 ambao umeanza kwa ushindani mkubwa na timu hiyo ilipata ushindi kwenye mchezo wake wa tatu baada ya kucheza dakika 180 bila kupata pointi tatu.

Ikumbukwe kwamba Nado ni mchezaji wa kwanza kupiga kona katika kikosi hicho ilikuwa Agosti 28 2024 dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Meja Isamuhyo alipiga dakika ya 56 katika mchezo huo ilikuwa 0-0 hivyo waligawana pointi mojamoja.

Azam FC ilicheza mechi mbili mfululizo ambazo ni dakika 180 bila kufunga na ilipachika bao kwenye mchezo wao dhidi ya KMC uliochezwa Septemba 19 2024.

Ni yeye anaingia kwenye orodha ya kuwa mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Azam FC dakika ya 19 dhidi ya KMC, Septemba 19 2024 ubao wa Uwanja wa KMC Complex ukisoma KMC 0-4 Azam FC.

Mchezaji wa kwanza kupewa kuku Uwanja wa KMC Complex  na mashabiki wa timu hiyo ni yeye Nado ambaye aliweka wazi kuwa furaha kubwa kwa timu hiyo kushinda mchezo huo.

“Furaha kubwa kwetu kupata pointi tatu kwenye mchezo wetu hivyo tunawashukuru mashabiki kwa kujitokeza katika mchezo wetu.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Dizo Click.