KMC YAKIRI KUFANYA MAKOSA MENGI UWANJANI

BENCHI la ufundi la KMC limebainisha kuwa kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge baada ya dakika 90 wakapoteza pointi tatu.

Ilikuwa KMC 0-4 Azam FC ambao walipata ushindi wa kwanza ndani ya ligi baada ya kucheza mechi mbili mfululizo bila kupata ushindi. Mechi za Azam FC ilikuwa JKT Tanzania 0-0 Azam FC, Azam FC 0-0 Pamba Jiji.

Abdi Himid Moallin ambaye aliwahi kuwa kocha ndani ya Azam FC ameweka wazi kuwa walifanya makosa kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa jambo lililowafanya wakapoteza pointi tatu.

“Tulikuwa na mpango kazi mkubwa wa kutafuta matokeo kwenye mchezo wetu lakini tulishindwa kutokana na kufanya makosa mengi ambayo tulifanya. Tunaamini tutafanyia kazi makosa yaliyotokea kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi zetu zijazo.”

Kocha Mkuu wa Azam FC Rachid Taoussi amesema ni furaha kwa wachezaji na timu kiujumla kupata matokeo kwenye mchezo wao wa ligi.

“Pongezi kwa wachezaji wamecheza vizuri na matokeo yamepatikana na hata mchezo uliopita dhidi ya Pamba tulicheza vizuri lakini hatukupata matokeo.’

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Dizo Click.