AZAM FC USHINDI WA 4G SALAMU KWA MNYAMA

BAADA ya ushindi wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara mbele ya KMC, Septemba 19 2024 uongozi wa Azam FC umeweka wazi kuwa hizo ni salamu kwa mpinzani wao ajaye ambaye ni Simba.

Azam FC ilishuhudia ubao wa Uwanja wa KMC Complex ukisoma KMC 0-4 Azam FC kwa mabao ya Idd Suleiman Nado dakika ya 19, Lusajo Mwaikenda dakika ya 55, Nassoro Saadun dakika ya 60 na Freddy Tangalo alijifunga dakika ya 67 katika harakati za kuokoa hatari kutoka kwa Nathaniel Chilambo.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo huo kiungo Feisal Salum alikuwa mchezaji bora alikomba dakika 90 na kutoa pasi mbili za mabao huku akipiga shuti moja ambalo lililenga lango.

Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema walibainisha wazi kuwa wanaanza ligi wapo ambao walikuwa wakibeza hivyo ushindi huo ni salamu kwa wapinzani wao wanaofuata.

 “Hapa ligi ndo imeanza rasmi salamu kwa ajaye na ratiba inaonyesha kwamba tutacheza na Simba hivyo wajipange. Huu mwendo ambao tumeanza nao inaonyesha ukubwa na uimara wa timu yetu hakika tunaamini kwamba tutafanya kazi kubwa.

“Wapinzani wetu KMC tumewachanganya wakiwa nyumbani kwao, tunawapongeza kwa kuwa tumecheza kwenye uwanja ambao unafanana na sehemu ambayo tumeizoea pale Azam Complex.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Dizo Click.