HII HAPA RATIBA YA MECHI ZA LEO KITAIFA NA KIMATAIFA

WIKIENDI ipo bize kitaifa na kimataifa kwa kila timu kuwa kazini kusaka ushindi ndani ya dakika 90 huku Ligi Kuu Bara ikiwa inaendelea na Ligi ya Mabingwa Afrika pia kama kawaida.

Wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa kwa sasa ni Yanga baada ya matajiri wa Dar, Azam FC kugotea kwenye hatua ya awali hivyo kazi imebaki kwa Yanga na katika Kombe la Shirikisho Simba Septemba 15 watakuwa na kazi nchini Libya huku Coastal Union wao wakibaki kuwa mashuhuda baada ya kugotea hatua ya awali.

Tukianza Bongo leo Septemba 14 2024 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo kutakuwa na mechi mbili kali ndani ya uwanja kwa kila timu kupambania ushindi baada ya dakika 90 kukamilka.

Tabora United itawakaribisha Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mchezo unatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni.

Azam FC inashuka uwanjani kwenye mchezo wa kwanza ikiwa Uwanja wa Azam Complex itakuwa saa 1:00 usiku na zote zitarushwa ndani ya Azam TV ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza kwa Azam FC kwenye ligi ilikuwa JKT Tanzania 0-0 Azam FC ulikuwa ni wa mwisho kwa Yusuph Dabo kuinoa timu hiyo.

Kwenye anga la kimataifa Yanga itakuwa nchini Ethiopia mchezo unaotarajiwa kuchezwa saa 9:00 alasiri ni CBE SA v Yanga kwa kila timu kusaka tiketi ya kusonga mbele hatua ya makundi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Dizo Click.