KAGERA Sugar inayotumia Uwanja wa Kaitaba kwenye mechi za nyumbani mambo ni magumu katika mechi tatu mfululizo ambazo ni dakika 270 kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25 kwa kukwama kupata matokeo chanya.
Mechi mbili ambazo ni dakika 180 walicheza Uwanja wa Kaitaba ilikuwa Kagera Sugar 0-1 Singida Black Stars, Kagera Sugar 0-2 Yanga na kete ya tatu ilikuwa Tabora United 1-0 Kagera Sugar, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mchezo wao wa kwanza kucheza ugenini.
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Paul Nkata ameweka wazi kuwa haikuwa rahisi kupata ushindi ugenini licha ya wachezaji wake kujitahidi kipindi cha pili.
“Wachezaji walijitahidi kupambana kusaka ushindi kipindi cha pili lakini haikuwa hivyo kwani kupata matokeo ugenini sio rahisi tuna amini makosa ambayo yametokea tutafanyia kazi kuwa imara kwa mechi zijazo.”
MATOKEO HAYA HAPA SEPTEMBA 11
Tabora United 1-0 Kagera Sugar, goal dakika ya 32 kwa mkwaju wa penalti mtupiaji Asiegbu Shedrack, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Fountain Gate 2-1 Ken Gold kwa Ken Gold mtupiaji ni Joshua Ibrahim dakika ya 9 na Fountain Gate ni Kassim Suleiman dakika ya 42 na Seleman Mwalimu dakika ya 58 Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati.
RATIBA SEPTEMBA 12
Singida Black Stars v KMC, saa 10:00 jioni, Uwanja wa Liti.
Dodoma Jiji v Namungo FC, saa 10:00 jioni, Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati saa 10:00 jioni.
SEPTEMBA 13 2024
Azam FC v Pamba Jiji, Azam Complex saa 1;00 usiku
SEPTEMBA 14
Tabora United v Tanzania Prisons saa 10:00 jioni.
SEPTEMBA 15 2024
Pamba Jiji v Singida Black Stars, saa 8:00 mchana.