NYOTA Simon Msuva anakwenda kuanza maisha mapya Ulaya katika timu iliyopo Jamhuri ya Iraq huko Asia wa msimu wa 2024/25.
Msuva ni miongoni mwa wachezaji wenye uwezo mkubwa uwanjani huku siri kubwa ikiwa ni mazoezi amekuwa akipenda kuona timu ya taifa ya Tanzania inapata matokeo mazuri kwenye mechi zote ambazo inacheza.
Katika mchezo uliopita wa kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Ethiopia uliochezwa Uwanja wa Mkapa nyota huyo hakuwa kwenye orodha ya wachezaji waliopo kambini ila aliweka wazi kuwa anazungumza na wachezaji wote kuhusu kupambania nembo ya Tanzania.
“Kila mchezaji ana nafasi ya kucheza timu ya taifa ya Tanzania, niwe nimeitwa ama sijaitwa bado ninaipenda timu ya taifa ya Tanzania kwa kuwa nipo Tanzania na nikiitwa lazima nipambane kuona tunapata matokeo.
“Wachezaji wote walioitwa huwa tunazungumza nao ikiwa ni pamoja na Clement Mzize, Wazir Junior, kukumbushana kuhusu umuhimu wa kushinda kwenye mechi za taifa. Ambacho huwa ninapenda nikifunga hapo dunia nzima inajua kwamba kuna Msuva amefunga ama mchezaji fulani amefunga hili ni jambo kubwa.
“Kuna timu nimepata hivyo mashabiki wasiwe na mashaka, haiwezi kuwa hivyo eti nikakosa kabisa timu hapana nitacheza tena kwa kuwa kazi yangu ni mpira.” Msuva alisema hayo hivi karibu.