JOB AJIPAKULIA MINYAMA YANGA KWA HILI

BEKI wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga, Dickson Job amesema kuwa ameandika rekodi yake nyingine mpya msimu wa 2024/25 kwa kutoa pasi ya kwanza katika Ligi Kuu Bara kwa kusema hivyo ni kama anajipakulia minyama hivi kwa kuwa rekod zinaonyesha aliyefanya hivyo ni Pacome.

Ipo wazi kuwa Agosti 29 2024 mabingwa mara 30 Yanga walicheza mchezo wa kwanza wa ligi baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 0-2 Yanga.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 25 na Mzize Clement dakika ya 88 ikiwa ni bao la jioni kwa Yanga msimu wa 2024/25.

Job alikuwa mfungaji wa bao la kwanza ndani ya ligi 2023/24 aliwafunga KMC, Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ulisoma Yanga 5-0 KMC kwenye mchezo wa mwanzo wa msimu wa 2024/25 amesema ameweka rekodi ya kuwa mtoaji pasi ya kwanza.

“Tukiwa tunacheza tunahitaji ushindi bila kujali nani atafunga kwani sisi ni timu na tunafanya kazi kwa kushirikiana ila unaona kwenye mchezo wa kwanza nimetoa pasi ya kwanza angalia vizuri.” alisema Job kwa utani huku akicheka.