>

AZAM FC HASIRA KIMATAIFA KUHAMIA KWA JKT TANZANIA

BRUNO Ferry, Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa wamefadhaishwa na matokeo dhidi ya APR ya Rwanda hivyo hasira zitahamia kwa JKT Tanzania.

Ipo wazi kuwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Azam FC wamefungashiwa virago na APR kwa jumla ya mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ilikuwa Azam FC 1-0 APR bao likifungwa na Blanco kwa mkwaju wa penalti iliyosababishwa na Feisal Salum.

Mchezo wa marudio uliochezwa Rwanda ilikuwa APR 2-0 Azam FC hivyo safari ya Azam FC ikawa imegota mwisho. Leo Agosti 28, Azam FC inatarajiwa kutupa kete ya kwanza katika Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2024/25.

Kocha huyo amesema: “Tumefedheheshwa na matokeo yetu dhidi ya APR ilikuwa ni tatizo kubwa hivyo tunaamini wachezaji wetu watafanya vizuri kwenye mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania. “

Mchezo wa mwisho 2023/24 walipokutana ubao wa Uwanja wa Meja Isamuhyo ulisoma JKT Tanzania 0-2 Azam FC mabao yakifungwa na Sopu, Feisal Salum.