>

SIMBA QUEENS YAPOTEZA KIMATAIFA

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimatafa Simba Queens wamepoteza mchezo wa nusu fainali kwa kufungwa mabao 3-2 dhidi ya Kenya Police Bullets uliochezwa Uwanja wa Abebe Bikila, Ethiopia.

Simba Queens ilikuwa inachuana kuwania tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao kupitia kwa kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

Kupoteza kwenye hatua ya nusu fainali kunaifanya timu hiyo kugota hapo hivyo itacheza mchezo wa kuwania kusaka mshindi wa tatu kabla ya kurejea kwenye ardhi ya Tanzania.

Bingwa wa mashindano ya Cecafa ndiye anayekamatia tiketi ya kufuzu michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa timu za wanawake.

Kenya Police Bullets imejihakikisha nafasi ya kutinga fainali ikiwa inasubiri mshindi baina ya CBE ya Ethiopia na Kawembe Muslim ya Uganda kwenye mchezo wa fainali na yule atakayepoteza nusu fainali  atacheza na Simba Queens msako wa mshindi wa tatu.

Ikumbukwe kwamba mabao yote mawili ya Simba yamefungwa na Vivian Corazone moja ilikuwa kipindi cha kwanza akiweka usawa na moja kipindi cha pili likiwa bao la kutangulia kwa Simba mwisho wakapoteza mchezo huo.

Licha ya kupoteza kwenye mchezo wa nusu fainali bao wachezaji walipambana kusaka matokeo hivyo ni muda wa kujipanga kwa wakati ujao.