SIMU ZITAITA SANA KWA MUDA

MUDATHIR Yahya kiungo wa Yanga ubora wake uleule unaendelea msimu wa 2024/25 kwa mujibu wa Maulid Kitenge ameweka wazi kuwa kwa Muda simu zitaita sana.

Agosti 4 katika utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwa na kikosi cha Yanga msimu wa 2023/24 kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 2-1 Red Arrows alipachika bao moja.

Dakika ya 64 aliweka usawa bao la Red Arrows ambalo lilifungwa kipindi cha kwanza kupitia kwa Ricky Banda dakika ya 5 kwa mabingwa wa Kagame Cup.

Bao la pili la ushindi kwa Yanga lilifungwa na Aziz Ki dakika ya 90 kwa pigo la penalti baada ya beki wa Red Arrows kumchezea faulo Nickson Kibabage.

“Kwa Muda simu zitaita sana kwa kuwa msimu uliopita ziliita ni mwendelezo wa furaha.” Kitenge.

Ipo wazi kuwa kwenye Wiki ya Mwananchi iliandikwa rekodi ya kujaza viwanja viwili kwa mpigo kwa mashabiki wa Yanga ambao walijitokeza kushuhudia tamasha hilo la sita kwa Yanga.

Uwanja wa Mkapa ilikuwa Full House na Uwanja wa Uhuru ilikuwa Full House.