MANCHESTER United imefunga 2021 kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu England na kusepa na pointi tatu.
Ni mabao ya Scott Mc Tominay dakika ya 8,Ben Mee dk 27 alijifunga na Cristiano Ronaldo dk 35 alutupia bao katika mchezo huo.
Ni Aaron Lennon dk 38 alipachika bao pekee kwa timu yake ya Burnley kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Old Trafford.
United inafikisha pointi 31 ikiwa nafasi ya 6 huku Burnley ikiwa na pointi 11 nafasi ya 18.