>

KIMATAIFA YANGA KUANZIA HATUA YA AWALI, AZAM FC AMA JKU KUKUTANA NAO

KAZI imeanza kwenye anga la kimataifa ambapo wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga na  Azam FC watatambua nani atakuwa nani kwenye kusaka ushindi ndani ya dakika 90.

Ni kwenye droo ya CAF leo Julai 11 2024 nchini Misri kuna hatihati Yanga ikakutana na Azam FC ama JKU kwenye hatua ya awali kwa kuwa wapo pot tofauti.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi na Pyramids watapangwa na timu zilizopo katika pot 1 hivyo timu hizi mbili hazitawezeka kukutana katika kusaka ushindi wa kusonga mbele kimataifa.

Miongoni mwa timu ambazo zipo kwenye Pot 1 zinazoweza kukutana na Yanga ni Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu Yusuph Dabo, JKU,  Vital’O, Arta Solar, Gor Mahia, APR, Dekadaha, SC Club Villa, El Merekh ya Sudan Kusini, Commercial Bank ya Ethiopia.

Kwa maana hiyo kama upepo utakuwa kwa timu za Tanzania kukutana basi kuna uwezekano wa Yanga kukutana na Azam FC ama JKU huku Prymids ikiwa na nafasi kubwa kukutana na Azam FC.

Simba na Castal Union hizi zina kazi ya kupeperusha bendera kwenye anga la kimataifa Kombe la Shirikisho.