CONFIRMED: MZAMIRU AONGEZA MIAKA MIWILI

Kiungo mkabaji wa Simba, Mzamiru Yassin amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia Msimbazi. Mkataba wa Mzamiru umemalizika mwishoni mwa msimu huu na mapendekezo ya kiufundi yamependekeza mchezaji huyo kubaki kutokana na mchango wake, hivyo uongozi wa Simba umemuongezea miaka mingine miwili ya kuendelea kusalia kikosini.