YANGA YAGOMEA KISASI, PILATO HUYU HAPA FAINALI

KUELEKEA katika mchezo wa fainali ya CRDB Federation Cup Juni 2 2024 kati ya Yanga dhidi ya Azam FC, mabingwa watetezi wamegomea kulipa kisasi.

Ipo wazi kuwa Yanga ni mabingwa watetezi wa taji hilo wanakumbuka walipokutana katika mchezo wa ligi mzunguko wa pili walipotoza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Mkapa.

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wanatambua mchezo wao utakuwa na ushindani mkubwa ila watapambana kucheza soka safi hawafikirii kuhusu kulipa kisasi.

Yanga ndiyo timu inayocheza soka safi zaidi Tanzania hilo lipo wazi lakini kuelekea mchezo wetu wa fainali tupo vizuri na hatuna mpango wa kulipa kisasi kwa kuwa mchezo wa mpira hauhitaji kulipizana visasi bali maandalizi.

“Ninaamini kwamba utakuwa mchezo wenye ushindani mkubwa hilo lipo wazi tutafanya kazi kubwa kwa kuwa wachezaji wapo tayari hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.”.

Mwamuzi wa mchezo huo wa fainali ni Ahmed Arajiga ambaye alikuwa pia ni mwamuzi kwenye Kariakoo Dabi mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Miongoni mwa wachezaji waliopo Zanzibar ni pamoja na Jonas Mkude, Maxi Nzengeli, Pacome, Aziz KI.