MWAMBA HUYU HAPA ATAJWA KUMALIZANA NA YANGA

 BEKI wa kazi ndani ya FC Lupopo Chadrack Boka anatajwa kumalizana na mabosi wa Yanga kwa ajili ya kuwa ndani ya timu hiyo msimu wa 2024/25.

Beki huyo mwenye miaka 24 raia wa DR Congo Yanga wanatajwa kumalizana naye mapema kwa ajili ya kuimarisha kikosi hicho kinachonolewana Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa wa ligi wakiwa na pointi zao 80 msimu wa 2023/24 beki wao wa upande wa kushoto chaguo la kwanza alikuwa ni Joyce Lomalisa ambaye anatajwa kwamba anasepa ndani ya kikosi hicho.

Sababu hiyo imewafanya mabosi wa Yanga kuingia chimbo kusaka mashine nyingine ya kazi mapema wamemalizana na beki huyo ambaye atakuja kuchukua mikoba ya Lomalisa.

Ni kandarasi ya miaka miwili inatajwa kwamba amesaini kujiunga na timu hiyo yenye tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.