>

FUNGA KAZI 2023/24 RATIBA HII HAPA

LIGI Kuu Tanzania Bara mzunguko wa pili wa funga kazi unatarajiwa kuwa Mei 28 2024 kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.

Ipo wazi bingwa ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi hesabu ni kwenye tuzo ya kiatu bora na nani atamaliza nafasi ya pili msimu wa 2023/24.

Mechi za mwisho ni maamuzi kwa kuwa tofauti ya Simba na Azam ni kwenye mabao ya kufunga ambapo mtaji wa Azam FC ni kwenye safu ya ushambuliaji yenye mabao mengi na ukuta haujaruhusu mabao mengi.

Hii hapa ratiba ya mzunguko wa pili raundi ya 30 upo namna hii:-

Simba dhidi ya JKT Tanzania

Geita Gold dhidi ya Azam FC

Yanga dhidi ya Tanzania Prisons

Namungo dhidi ya Tabora United

Coastal Union dhidi ya KMC

Ihefu dhidi ya Mtibwa Sugar

Singida Fountain Gate dhidi ya Kagera Sugar