MMNYAMA NA BALAA LAKE MBELE YA DODOMA

MNYAMA Simba ameandika rekodi yake kwa kupata ushindi dakika zote 720 walipokutana na Dodoma Jiji katika mechi za ligi.

Tangu mwaka 2021 Klabu ya Dodoma Jiji haijapata ushindi mbele ya Mnyama Simba katika mechi za Ligi Kuu Bara kwenye jumla ya mechi 8 zote ilikuwa ushindi kwa Simba.

Ikumbukwe kwamba mchezo uliopita dhidi ya Dodoma Jiji ulikuwa ni mchezo wa kwanza ndani ya ligi kwa kipa Hussen Abel ambaye aliibuka ndani ya Simba akitokea KMC.

Dakika 90 Mei 17 alikamilisha akishuhudia ubao wa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ukisoma Dodoma Jiji 0-1 Simba ambapo bao pekee la Simba lilifungwa na Michael Fred dakika ya 7.

Pointi 60 Simba inafikisha baada ya mechi 27 ikiwa nafasi ya tatu sawa na Azam FC iliyo nafasi ya pili tofauti katika mabao ya kufunga na kufungwa.

Dodoma Jiji ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 27 msimu wa 2023/24.

Mchezo ujao wa ligi kwa Simba ni dhidi ya Geita Gold unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Mei 21 ikiwa ni mzunguko wa pili.