MATAJIRI wa Dar Azam FC chini ya Kocha Mkuu Yusuph Dabo wamefanikisha lengo la kutinga hatua ya fainali CRDB Federation Cup kwa ushindi wa mabao 3-0 Coastal Union.
Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, Azam FC wamekuwa wababe ndani ya dakika 90.
Mabao mawili yamefungwa na Abdul Sopu ilikuwa dakika ya 42 kwa mkwaju wa penalti na bao la pili ilikuwa dakika ya 79 alifunga.
Kiungo Feisal Salum alipachika bao moja dakika ya 68 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Ikumbukwe kwamba Sopu baada ya kuwafunga Coastal Union aliwaomba msamaha kwa kuwa ni timu aliyokuwa akicheza kabla ya kuibukia ndani ya Azam FC.
Mshindi wa mchezo kati ya Yanga dhidi ya Ihefu atakutana na Azam FC kwenye mchezo wa fainali.