COASTAL UNION KUMENYANA NA AZAM FC

WANAUME wa kazi Azam FC na Coastal Union wanatarajiwa kuvuja jasho ndani ya dakika 90 kusaka mshindi atakayetinga fainali kwenye mchezo wa CRDB Federation Cup hatua ya nusu fainali dhidi ya Azam FC.

Ni Uwanja wa CCM Kirumba mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwa timu hizo mbili kuwa na kazi kusaka ushindi.

Ni mchezo unaotarajiwa kumtoa mshindi atakayetinga hatua ya fainali ambapo atamsubiri mshindi kati ya mchezo wa Yanga dhidi ya Ihefu unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha Mei 19 2024.

Azam FC ilianza kupata ushindi wa mabao 2-1 Alliance raundi ya pili, Azam FC 5-0 Green Warriors raundi ya tatu, Azam FC 3-0 Mtibwa Sugar raundi ya nne na katika robo fainali iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 Namungo.

Leo Mei 18 2024 mchezo huo unatarajiwa kwa wababe hao wawili kukutana uwanjani kusaka mshindi atakayetinga hatua ya fainali.

Kwa upande wa Coastal Union wao ilikuwa Coastal Union 2-0 Greenland, Coastal Union 1-0 Mbeya Kwanza, Coastal Union 0-0 JKT Tanzania ikashinda kwa penalti 5-4 katika raundi ya nne na robo fainali ilikuwa Coastal Union 1-0 Geita Gold.

Miongoni mwa wachezaji wa Azam FC waliopo kwenye maandalizi ya mwisho ni pamoja na kinara wa utupiaji kwenye kikosi hicho kwenye ligi Feisal Salum akiwa na mabao 15.