FUNGAFUNGA BADO MBILI SIMBA

SIMBA inafikisha pointi 60 baada ya kucheza mechi 27 nafasi ya tatu ikiwa sawa pointi na Azam FC iliyo nafasi ya pili tofauti kwenye mabao ya kufunga na kufungwa.

Michael Fred ambaye Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba Ahmed Ally anapenda kumuita fungafunga amebakisha mabao mawili kufikia rekodi ya mwamba Jean Baleke na mechi zimebaki tatu kwa Simba kukamilisha mzunguko wa pili.

Ni bao alilofunga dhidi ya Dodoma Jiji kwake linakuwa ni bao la sita ndani ya ligi akiwa namba mbili kwa wakali wenye mabao mengi ndani ya kikosi hicho kwa kuwa Saido Ntibanzokiza na Clatous Chama wametupia mabao 7 kila mmoja.

Jean Baleke alipewa mkono wa asante akiwa katupia mabao 8 msimu wa 2023/24.

Ipo wazi kwamba vita ya ubingwa imegota mwisho na sasa ni kushuka daraja pamoja na nani atagotea nafasi ya pili kwenye msimamo.

Simba na Azam FC zinagombea nafasi ya pili zote zimekusanya pointi 60 huku vita nyingine ikiwa ni kwenye kiatu cha ufungaji bora Aziz KI wa Yanga na Feisal Salum wa Azam FC wote wametupia mabao 15.