>

YANGA WANATARAJIWA KUTANGAZWA KUWA MABINGWA WA LIGI KUU KWA MARA YA 30

Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara inaendelea tena leo Mei 13, 2024 huku macho na masikio yakielekezwa katika dimba la Manungu Complex, Turiani Morogoro ambapo Wananchi wanatarajiwa kutangazwa kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya 30 kihistoria ikiwa watachukua pointi tatu dhidi ya Wakata Miwa.

16:00 | Mtibwa Sugar vs Yanga Sc
🏟️ Manungu Complex, Morogoro

Yanga Sc wakishinda watafikisha alama 71 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote kwa mechi zilizosalia kabla ya kufungwa kwa pazia la Ligi.

Azam Fc waliopo nafasi ya pili wakishinda mechi tatu zilizosalia watafikisha pointi 69 sawa na Simba Sc ambao watafikisha pointi 69 wakishinda michezo yao minne iliyobaki.

MSIMAMO 🔝3️⃣
🥇Yanga Sc — mechi 26 — pointi 68
🥈 Azam Fc — mechi 27 —pointi 60
🥉 Simba Sc —mechi 26— pointi 57