MTIBWA SUGAR SIO KINYONGE YAFANYA KWELI

KUTOKA Morogoro, Mtibwa Sugar baada ya kucheza mechi 26 wamekusanya alama 20 msimu wa 2023/24 wakiwa nafasi ya 16.

Zuber Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amebainisha kuwa watafanya kazi kubwa kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi ambazo watacheza.

“Tuna kazi kubwa kwenye mechi zetu ambazo tunacheza kikubwa ni kutumia nafasi ambazo tunapata na kuwa makini kujilinda tusifungwe, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.”.

Mtibwa Sugar ipo katika mstari wa kushuka daraja ikiwa itashindwa kupata matokeo chanya katika mechi zake nne zilizobaki kwa wakati huu kumaliza mzunguko wa pili.

Ni mechi 5 pekee imeshinda sawa na idadi ya sare huku ikipoteza jumla ya mechi 16 ikiwa timu namba moja kupoteza mechi nyingi.

Pia safu yake ya ulinzi imeokota jumla ya mabao 43 ikiwa namba moja kwa timu iliyofungwa mabao mengi huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao 26 Ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 90.

Mei 9 2024 walisepa na pointi tatu mazima dhidi ya Tabora United kwa ushindi wa mabao 3-0, Uwanja wa Manungu.

Mabao ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Jimson Mwanuke, Ilanfya na Nickson Mosha (Kasami) kutoka timu ya vijana ikiwa ni bao  lake la kwanza la ligi.