Skip to content
KLABU ya AL Ahly imetimga hatua ya fainali Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifungashia virago TP Mazembe ya DR Congo.
AL Ahly imeshinda jumla ya mabao 3-0 TP Mazembe katika mchezo wa nusu fainali ya pili mabao yote yalifungwa.
Ilikuwa dakika ya 68 kupitia kwa Mohamed Abdelmonem, Wessam Abou Ali dakika ya 83 na Akram Tawfik dakika ya 90.
Hivyo itakutana na ES Tunis iliyowafungashia virago Mamelodi Sundowns kwa kuwapiga nje ndani ikiwa ni jumla ya mabao 2-0.
Mamelodi yamewakuta Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutinga kwenye hatua hiyo kwa utata wa bao la Aziz KI wamekwama kufunga mwanzo mwisho.
Ikumbukwe kwamba kuanzia hatua ya robo fainali safu ya ushambuliaji haikufunga na kwenye nusu fainali pia.
Dakika 180 nje ndani itakuwa Mei ambapo ES Tunis wataanza wakiwa nyumbani na fainali ya pili itakuwa Misri kati ya Aprili 25.
Al Ahly waliwafungashia virago Simba kwenye hatua ya robo fainali wao ni mabingwa watetezi.