FAINALI YA MUUNGANO KUPIGWA NA HAWA HAPA

KOMBE la Muungano 2024 limeanza kuunguruma Visiwani Zanzibar ambapo limeanzia kwenye hatua ya nusu fainali.

Nusu fainali ya kwanza ilikuwa ni Aprili 24 2024 ambapo ilikuwa ni Uwanja wa New Amaan Complex.

Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma KVZ 0-2 Simba hivyo Simba inakuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya fainali.

Mchezo wa pili wa nusu fainali ni Aprili 25 2024 itakuwa Azam FC dhidi ya KMKM ambapo mshindi wa mchezo wa leo atatinga fainali kukutana na Simba.

Fainali ya Muungano inatarajiwa kuchezwa Aprili 27 kwa wababe wawili kusaka mshindi ndani ya uwanja kwa msimu wa 2024.