INONGA KWENYE ULIMWENGU WAKE SIMBA

HENOCK Inonga katika Ligi Kuu Bara sio chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Abdelhakh Benchikha kwa kuwa anatumia muda mwingi nje ya uwanja.

Beki huyo yupo kwenye ulimwengu wake mwenyewe kutoakana na kutokuwa kwenye ubora wake katika mechi ambazo wanacheza msimu huu.

Msimu wa 2023/24 umekuwa ni mbaya kwake baada ya kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union September 21 2023 alipotumia dakika 19 tu.

Lakini Inonga akiwa na timu ya taifa ya DR Congo anavaa uhalisia wa sura ya kazikazi jambo ambalo limekuwa likitajwa kuwavutia mabosi wa timu nyingi zinazohitaji kuinasa saini yake.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa pili Kariakoo Dabi dhidi ya Simba alikwama kukamilisha dakika 90 baada ya kupata maumivu kipindi cha kwanza.

Nafasi yake ilichukuliwa na Hussein Kazi ambaye alifanya makosa yaliyoigharimu timu hiyo kufungwa bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti na Aziz KI kwa kuwa alisababisha faulo beki huyo.