KLABU ya Geita kwa sasa haitaki utani baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji wakongwe na wenye uzoefu kwenye fani.
Miongoni mwa wachezaji ambao watakuwa na uzi wa timu hiyo ni pamoja na nyota wa zamani wa Yanga na Polisi Tanzania, Kelvin Yondani, ambaye amesaini dili la mwaka mmoja Geita Gold, mkataba utakaomfanya kuziba safu ya ulinzi sambamba na Juma Nyosso ambaye tayari ameingia kwenye klabu hiyo.
Yondani aliachana naYanga mwanzoni mwa msimu wa 2019/20 na baadaye akajiunga na Polisi Tanzania baada ya kupita miezi sita mkataba uliodumu kwa mwaka mmoja kabla ya kuamua kujiunga na Geita Gold.
Ofisa Habari wa Geita Gold, Hemed Kivuyo, amesema, ni kweli Yondani ataungana na Juma Nyosso msimu huu baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja, kwani wao wameamua
kutengeneza ukuta wa kudumu ili waweze kufikia malengo yao.
“Tarifa ya faraja kwetu ni uwepo wa wachezaji hawa wazoefu, kwani ni kweli Yondani atakipiga msimu huu sambamba na Nyosso ikiwa ni sehemu ya maboresho ya safu yetu ya ulinzi.
“Mbali na hivyo pia tayari tumefanikiwa kumsaini Ditram Nchimbi, hivyo utaona hitaji la timu yetu lilikuwa ni kupata zaidi wachezaji wenye uzoefu na ligi ili tuweze kufikia male, pamoja na wote kusaini mwaka mmoja mmoja, ni wazi kwamba kama watatuwezesha kufikia malengo yetu ni wazi wataongeza tena,” amesema Kivuyo.
Pia Luccian William naye pia amejiunga na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Felix Minziro.
Wakati huohuo, uongozi wa timu ya Geita Gold FC umethibitisha kuingia mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) wenye thamani ya Sh milioni 500