BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa suala la afya kwa wachezaji ni muhimu mbali na kuwa na kikosi kipana. Wachezaji wa Simba walikwama kucheza mchezo wao wa ligi dhidi ya Kagera Sugar uliotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kaitaba, Desemba 18 hivyo utapangiwa tarehe.
Leo Desemba 24 kikos cha Simba kitakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya KMC, Uwanja wa Ali Hassan Miwnyi,Tabora ambapo Barbara amesema kuwa wanahitaji pointi tatu.