Skip to content
MSAFARA wa Simba umewasili Misri tayari kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 5 2024 Uwanja wa Taifa wa Cairo na mshindi wa jumla atatinga hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ikumbukwe kwamba kàtika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 0-1 Al Ahly.
Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Ayoub Lakred, Kibu Dennis, Hussen Abel, Henock Inonga.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo