MKWANJA MEZANI WAWEKWA NA CRDB BILIONI 3

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Benki ya CRDB, wamesaini mkataba wa udhamini wa Kombe la Shirikisho ambapo awali lilikuwa linaitwa Azam Sports Federation sasa litakuwa ni CRDB Bank Federation Cup wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 kwa miaka mitatu na nusu

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameweka wazi kuwa malengo makubwa ni kuona kwamba mpira unaendelea kuwa na manufaa na wale ambao wanadhamini hawatajutia kuwa kwenye eneo hilo kwa kuwa watapata faida kubwa.

Jambo hili ni kubwa kwa kuwa linazidi kuogeza ushindani kwenye mashindano haya ambapo kila timu itaongeza nguvu kupambania kombe na bingwa mtetezi kwa sasa ni Yanga anayepambana kutetea taji hilo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alikuwa ni miongoni mwa wa waliokuwa kwenye hafla hiyo na walibadilishana mkataba wa udhamini wa Kombe la Shirikisho (CRDB Bank Federation Cup) uliosainiwa Aprili 2 2024 Makao Makuu ya CRDB, Dar es Salaam.

Pia katika suala la utiaji saini mkataba huo mbele ya Waandishi wa Habari Karia na Nsekela walihusika kwenye kusaini dili hilo.