KOCHA SIMBA KWENYE MTIHANA MZITO

KOCHA wa Simba, Abdelhak Benchikha yupo kwenye mtihani mzito kutokana na kutokuwa na washambuliaji wenye uwezo unaowapa nafasi kikosi cha kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pia washambuliaji wa Simba hawajawa tegemeo kwenye mechi za ligi jambo ambalo limewafanya wasiwe chaguo la kwanza kwenye mechi za hivi karibuni ndani ya uwanja.

Ikumbukwe kwamba washambuliaji waliopo ni Michael Fred na Pa Jobe hawajawa kwenye mwendo mzzuri kwenye mechi ambazo wamekuwa wakipata kuanza.

Baada ya mchezo dhidi ya Al Ahly, Benchikha aliweka wazi kuwa wanahitaji kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi kubwa na kuwapongeza wachezaji wake.

“Kupoteza mchezo dhidi ya Al Ahly haikuwa malengo yetu tumeona wapinzani wetu namna walivyocheza ile ni timu kubwa ipo wazi na ina wachezaji wenye uwezo mkubwa nasi tunahitaji wachezaji wenye uwezo mkubwa katika kuendeleza ushindani.

“Makosa ambayo tumefanya tutafanyia kazi kwa kuwa wachezaji wanafanya kazi kubwa kutimiza majukumu yao hilo linatupa nguvu kuamini kwamba tutafanya vizuri,’.

Mchezo ujao kwa Simba dhidi ya Al Ahly itakuwa ugenini, Aprili 5 2024.