YANGA YAKWEAA PIPA KUWAFUATA MAMELODI

KUELEKEA mchezo wa mkondo wa pili Mamelodi Sundowns dhidi ya Yanga, wawakilishi kutoka Tanzania Yanga wamewafuata wakiwa kamili gado.

Kàtika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 0-0 Mamelodi Sundowns hivyo dakika 90 za ugenini zitaamua nani atasonga mbele hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwenye msafara wa Yanga miongoni mwao ni pamoja na Pacome Zouzoua ambaye hakuwa sehemu ya kikosi kilichowakabili Mamelodi Sundowns, Uwanja wa Mkapa kwa kuwa bado hakuwa fiti asilimia 100.

Mbali na Pacome mwamba Joyce Lomalisa, Maxi Nzengeli, Bakari Mwamnyeto, Sure Boy ni miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ulioanza safari alfajiri ya Aprili 2.

Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania kimataifa.