WAARABU wa Misri, Al Ahly wameacha balaa zito ndani ya Simba kutokana na kuwaduwaza Uwanja wa Mkapa wakisepa na ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali.
Kazi kubwa kwa Simba ni kupambana kusaka ushindi kwenye mchezo wa mkondo wa pili unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Taifa wa Cairo Aprili 5 2024. Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa watafanyia kazi makosa yao ili kupata matokeo mchezo ujao.