UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa unawajali mashabiki na hauna tamaa ya fedha hivyo wameamua kupunguza viingilio kwenye kila sehemu huku wakiondoa kabisa upande wa mzunguko.
Yanga inatarajiwa kuwa na kazi kusaka ushindi Machi 30 mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambapo tayari maandalizi yameanza kufanyika.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema:”Wote tunakubaliana mechi ya Mamelodi ni mechi kubwa zaidi kwenye robo fainali ya CAFCL msimu huu na Viingilio ni kama vifuatavyo:
VIP C 10,000, VIP B 20,000, VIP A 30,000.
“Tunafahamu mechi itaisha usiku sana, kwa kuwajali mashabiki wetu na dhamira ya nchi yetu hasa kwenye sekta ya michezo. Viongozi wetu wameamua jukwaa mzunguko itakuwa bure,”.