>

TAIFA STARS SAFARINI KUELEKEA AZERBAIJAN

BAADA ya Hemed Morocco kutangaza orodha ya wachezaji watakaokuwa katika timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, safari imeanza kwa ajili ya kuelekea Azerbaijan ambapo wanatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki.

Tayari kikosi cha Taifa Stars kimewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Istanbul, Uturuki muda wowote kitakwe pipa kuelekea Baku, Azerbaijan kwenye mashindano ya FIFA Series.

Wakiwa nchini humo Stars watacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Bulgaria na Mongolia.

Mapema Machi 18 wachezaji wa Timu ya Taifa, Taifa Stars walianza safari kutoka uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa safari ya kuelekea Azerbaijan kwa michezo miwili ya FIFA Series 2024.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara ni pamoja na Bakari Mwamnyeto, Mudathir Yahya, Feisal Salum.