Arsenal wamepangwa dhidi ya Bayern Munich katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, huku Manchester City wakicheza na Real Madrid.
The Gunners watakuwa wenyeji wa Bayern ya Ujerumani, ambao wana nahodha wa Uingereza Harry Kane kwenye kikosi chao, kwenye Uwanja wa Emirates katika mechi ya kwanza.
Wakati huo huo, huu ni msimu wa tatu mfululizo kwa City kukutana na Real ya Uhispania katika hatua ya mtoano.
Mechi za kwanza zitafanyika Aprili 9-10, na za pili Aprili 16-17.
Iwapo Arsenal na City watashinda mechi zao klabu hizo mbili za Premier League zitamenyana katika nusu fainali.
Droo ya robo fainali
Arsenal v Bayern Munich
Atletico Madrid v Dortmund
Paris St-Germain v Barcelona
Real Madrid v Manchester City
Droo ya nusu fainali
Atletico Madrid au Borussia Dortmund v Paris St-Germain au Barcelona
Arsenal au Bayern Munich v Real Madrid au Manchester City