GAMONDI NA MTEGO WAKE KWA MZIZIMA DABI

MIGUEL Gamondi alianza na kiungo Mudathir Yahya kwenye benchi wakati ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Yanga 1-0 Geita Gold.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja Azam Complex kulikuwa na mabadiliko katika kikosi cha kwanza ikiwa ni maalumu kwa ajili ya kuwapa muda wachezaji wengine ambao hawakupata nafasi kucheza mechi zilizopita.

Mtego kwa Azam FC ambao wanatarajiwa kukutana nao Machi 17 2024 Uwanja wa Mkapa ipo wazi kwamba Muda katika mechi ambazo zilipita alianza kikosi cha kwanza.

Wengine ambao walikuwa benchi ni Clement Mzize, Pacome, Yao, Skudu Makudubela na walipata nafasi ya kuingia kipindi cha pili kwenye mchezo huo.

Bao la ushindi lilifungwa na Aziz Ki dakika ya 28 linamfanya afikishe mabao 13 hivyo mtego ilikuwa ni kuwapa muda wa kuvuta kasi baadhi ya wachezaji kuelekea mchezo huo.

Pointi 52 Yanga nafasi ya Kwanza huku Azam FC ikiwa nafasi ya pili na pointi 44.