FEI TOTO KASI YAKE YAONGEZEKA, AZAM YAPETA

KIUNGO mzawa mali ya Azam FC Feisal Salum MWENYE jumla ya mabao 11 katika orodha ya watupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara anazidi kuonyesha ubora wake kwa vitendo uwanjani.

Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Machi 3 2024 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 4-1 Dodoma Jiji na Fe alitupia mabao mawili.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 28, Feisal dakika ya 63, 64, Kipre Junior dakika ya 69 na Emmanuel Martin alifunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 84.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 43 kibindoni msimu wa 2023/24 sawa na vinara Yanga wakitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Kiungo huyo anaongoza chati ya watupiaji kwa sasa akifuatiwa na Aziz KI wa Yanga mwenye mabao 10.