BOSI SIMBA AMEWACHANA YANGA ISHU YA KUTINGA ROBO FAINALI

YANGA imeandika rekodi ya kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Machi Mosi na tayari kikosi cha Yanga kimewasili nchini Misri kwa ajili ya mchezo huo. Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa kutinga robo fainali kwa Yanga Mo anahusika.