AZAM FC WANAJIPANGA UPYA HUKO

MATAJIRI wa Dar, Azam FC wanajipanga upya kurejea kwenye ushindani baada ya kukosa matokeo kwenye mechi za hivi karibuni ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa mpango mkubwa kwenye mchezo wao dhidi ya Tabora United pamoja na mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons lakini ilishindikana kutokana na ushindani kuwa mkubwa.

Ipo wazi kwamba kwenye mechi mbili mfululizo matajiri hao wa Dar waliambulia pointi mbili kati ya msako wa pointi sita ugenini wakiyeyusha pointi nne jumlajumla.

Azam FC kwenye msimamo ipo nafasi ya pili baada ya kucheza jumla ya mechi 17 imekusanya pointi 37 vinara ni Yanga wakiwa na pointi 43 baada ya kucheza mechi 16.

Februari 25 Azam FC ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Sokoine Mbeya ukisoma Tanzania Prisons 1-1 Azam FC baada ya kukamilisha dakika 90 za Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Februari  19 kusoma Tabora United 0-0 Azam FC.

Dabo amesema: “Kwenye kila mchezo tulikuwa na mbinu tofauti ambazo tulikuwa tunazitumia na malengo ilikuwa ni kupata ushindi mwisho tumekosa, makosa ambayo yametokea tutayafanyia kazi hasa kwenye eneo la ushambuliaji ili kupata matokeo kwenye mechi zinazofuata,”.