TABORA UNITED WATUMA UJUMBE HUU AZAM FC

KOCHA Mkuu wa Tabora United, Goran Kopunovic amebainisha kwamba mchezo wao dhidi ya Azam FC hautakuwa mwepesi kutokana na wapinzani wao kuwa imara kwenye kusaka matokeo.

Ipo wazi kuwa Azam FC ipo nafasi ya tatu mchezo wao uliopita wa kufunga mzunguko wa kwanza walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Geita Gold mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Tabora United mchezo wake uliopita ilitoshana nguvu na Namungo FC jambo linaloongeza ushindani kwenye mchezo wa leo.

Kocha huyo amesema:” Ni moja ya mchezo ambao utakuwa ni mgumu kwa kuwa tunawatambua wapinzani wetu sio wepesi lakini katka hayo tumefanya maandalizi kupata matokeo.

“Wachezaji wapo tayari na tutaingia kwenye mchezo huo kwa tahadhari ili kupata matokeo mazuri ambayo yatatufanya tuzidi kuwa kwenye ushindani,”.

Azam FC kinara wao wa mabao ni Feisal Salum mwenye mabao 8 kibindoni ndani ya Ligi Kuu Bara timu yake ya kwanza kuifunga ilikuwa ni Tabora United, Uwanja wa Azam Complex.