>

SIASA YAMPONZA NYOTA WA BAFANA BAFANA MOKOENA, AKATALIWA AL AHLY

Klabu ya Al Ahly ya Misri imeahirisha mpango wake wa kumpa nafasi ya majaribio nyota wa Bafana Bafana, Tenoho Mokoena.

Katika taarifa yao ya leo, Al Ahly wamesema wamefikia uamuzi huo kutokana na misimamo ya kisiasa ya mchezaji huyo.

Hivi karibuni wakati Bafana Bafana wakirejea nyumbani kutoka Ivory Coast kwenye AFCON ambako walimaliza katika nafasi ya tatu, Mokoena alielezea mapenzi yake kwa Julius Malema, Rais wa chama cha upinzani cha EFF cha Afrika Kusini.

Katika taarifa yao, Al Ahly wamesema wamesikitishwa na Mokoena kumuunga mkono Malema ambaye anahubiri chuki yakiwemo mauaji dhidi ya wazungu wa Afrika Kusini.

Majaribio ya Mokoena klabuni Al Ahly yalipangwa kufanyika mwezi ujao lakini sasa ni hadi itakapoamriwa vinginevyo.