Skip to content
MATAJIRI wa Dar Azam FC wanazipigia hesabu pointi tatu za Geita Gold kuelekea mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Februari 16 Uwanja wa Azam Complex.
Yusuph Dabo, Kocha Mkuu wa Azam FC mchezo wake uliopita ilikuwa ni kiporo ambapo waligawana pointi mojamoja na Simba.
Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba ulisoma Simba 1-1 Azam FC na bao la Azam FC lilifungwa dakika ya 14 na Prince Dube.
Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zote na kikubwa wanahitaji pointi tatu muhimu.
“Tunatambua ushindani ni mkubwa tupo tayari ambacho tunahitaji kwenye mechi zetu ni kupata pointi tatu muhimu ndani ya uwanja wachezaji wapo tayari,”