ISHU YA SARE DHIDI YA AZAM FC SIMBA WAJA NA HILI HAPA

BAADA ya kuambulia sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC, mabosi wa Simba wamekuja na mpango kazi kwa ajili ya mechi znazofuata.

Ipo wazi kuwa Februari 9 ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba ulisoma Simba 1-1 Azam FC.

Prince Dube alipachika bao dakika ya 14 huku Clatous Chama akifunga bao la kuweka usawa dakika ya 90.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema:”Tunamshukuru Mungu kwa matokeo tuliyopata, Si mazuri sana na si mabaya sana

Tunawapongeza wachezaji wetu kwa kupambana na kuvuna alama moja kwani bila upambanaji wao tusingeipata

“Hili limekwisha, Sasa tunaangalia zaidi mechi ijayo. Asanteni Mwanza, Asante kanda ya Ziwa, Asanteni wana Simba. Jicho letu sasa ni Feb 12 dhidi ya Geita Gold hapa hapa Kirumba,”.

Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi 30 Azam FC nafasi ya pili na pointi 32.