UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kuna ofa kibao ambazo zinahitaji saini ya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Aziz KI raia wa Burkina Faso ambaye ni namba moja kwenye upande wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa katupia mabao 10 kibindoni sawa na namba ya jezi yake.